Nao ni upande unaolenga kutia nguvu Imani ya mja kwa Mola wake, kupitia kujua majina ya Mwenyezi Mungu na sifa Zake, na kuwatanabahisha watu watazame alama za Mwenyezi Mungu katika ulimwngu Wake, jambo ambalo litapelekea kuzifungamanisha nyoyo za waja na Mola wao kwa kumtegemea Yeye na kuogopa mateso Yake na kutaraji malipo mazuri kutoka Kwake, ili mja aishi maisha ya utulivu yaliyojaa Imani na kuridhika